Ezekiel 23:32-34

32 a“Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo:

“Utakinywea kikombe cha dada yako,
kikombe kikubwa na chenye kina kirefu;
nitaletea juu yako dharau na dhihaka,
kwa kuwa kimejaa sana.
33 bUtalewa ulevi na kujawa huzuni,
kikombe cha maangamizo na ukiwa,
kikombe cha dada yako Samaria.
34 cUtakinywa chote na kukimaliza;
utakivunja vipande vipande
na kuyararua matiti yako.
Nimenena haya, asema Bwana Mwenyezi.

Copyright information for SwhNEN